05. Qur-aan na Sunnah imetatua kila kitu

Kupitia haya inapata kufahamika kuwa ndani ya Qur-aan na Sunnah kumetatuliwa matatizo yote, kumebainishwa yale yote anayoyahitajia watu katika dini yao na kuhukumu magomvi yao. Kama ambavo katika hayo kuna nusura kwa mlinganizi wa haki na kumsambaratisha mpinzani wake kwa hoja za wazi. Kwa ajili hiyo amesema (Subhaanah):

وَلَا يَأْتُونَكَ بِمَثَلٍ إِلَّا جِئْنَاكَ بِالْحَقِّ وَأَحْسَنَ تَفْسِيرًا

“Wala hawakujii kwa mfano wowote isipokuwa Tunakuletea haki na tafsiri nzuri kabisa.”[1]

Mfano unaenea kila hoja tata wanayoitanguliza wanayodai kuwa ni hoja, madhehebu wanayodai kuwa ni sahihi na ulinganizi wanaodai kuwa ni wenye faida. Yote hayo yanafichuliwa na Kitabu hiki na zile Sunnah zilizoletwa na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Matatizo, hoja tata, madai yanayopotosha na fikira zote za kuangamiza wanazotanguliza, yote hayo yanafichuliwa na elimu kwa Kitabu hiki na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 25:33

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamiyyat-ul-´Ilm https://binbaz.org.sa/discussions/33/اهمية-العلم-في-محاربة-الافكار-الهدامة
  • Imechapishwa: 16/03/2022