Kama Qur-aan na Sunnah vingelikuwa havina mwongozo na kutoshelezeka, basi watu wasingerejea kwavyo. Isitoshe kurejea kwavyo kusingelikuwa na faida yoyote – Allaah ametakasika kutokamana na hayo utakasikaji mkubwa. Hakika si venginevyo watu wanarejea kwavyo wakati wa mzozo na kutofautiana kutokana na ule mwongozo, ubainifu wa wazi, kutatua matatizo na kuteketeza batili iliyomo ndani yavyo. Kisha akataja kuwa hiyo ni sharti ya imani pale aliposema (Subhaanah):

إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ

“… mkiwa mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho… “[1]

Kisha akataja kwamba kufanya hivo ndio kheri kwa waja duniani na Aakhirah na mwisho mema. Kwa msemo mwingine kuyarudisha kwa Allaah na kwa Mtume yale wanayozozana juu yake ndio kuna kheri kwao duniani na Aakhirah na kuna mwisho mwema kwao.

[1] 04:59

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamiyyat-ul-´Ilm https://binbaz.org.sa/discussions/33/اهمية-العلم-في-محاربة-الافكار-الهدامة
  • Imechapishwa: 16/03/2022