Ambaye anasoma na anaipenda elimu atakuja kujenga maktabah bila hata yeye kuhisi jambo hilo. Pengine akaiona Hadiyth iliyorejeshwa katika kitabu fulani, ambapo akajiambia nafsi yake kwamba ni lazima kwake kununua kitabu hicho. Wakati nilipoandika kitabu  ”at-Twaliy´ah fiyr-Radd ´alaa Ghullaat-ish-Shiy´ah”, nilikuwa na kikabati na nilikuwa nadhani kuwa kimejaa vitabu vya ulimwengu mzima. Wakati nilipokuwa naandika na nikaona kuwa nahitajia baadhi vya vyanzo vingine ambapo nikapatiliza kuvipata. Kisha baada ya hapo, wakati nilipoanza kuandika ”as-Swahiyh al-Musnad min Asbaab-in-Nuzuul”, nikaona kuwa maktaba yangu bado ni pungufu. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye ambaye anawepesisha bei za vitabu hata kama utalazimika kuchukua mkopo kwa ajili ya kununua kitabu. Wakati mmoja nilikuwa nataka kununua kitabu “Tadhiyb-ut-Tahdhiyb” cha Haafidhw Ibn Hajar. Kilikuwa kinauzikana 200 SAR. Kindi hicho nilikuwa Makkah na nikamuomba rafiki yangu anikope kiwango fulani cha pesa. Akaniuliza nini ninachotaka kuzifanyisha pesa hizo. Nikamwambia kuwa nataka kununua kitabu. Akasema hapana. Akasema kama ingelikuwa ni kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani au nguo, basi angenikopesha – lakini sio kwa ajili ya kununua kitabu. Tahamaki akashtuka kuona nina kitabu. Akaniuliza ni wapi nimekitoa? Nikamwambia kuwa Allaah (Subhaaahu wa Ta´ala) amesahilisha. Vinginevyo ni ndugu kwa ajili ya Allaah. Anatupenda kwa ajili ya Allaah  – Allaah amjaze kheri. Wakati mtu anapotilia umuhimu vitabu, basi Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anamsahilishia navyo.

Sitaki ukusanye vitabu kwa ajili tu ya pambo, kama wanavofanya baadhi ya watu. Niliwatemebelea baadhi ya Ahl-us-Sunnah na kuona katika maktaba zao kuna vitabu vipya, lakini ni kama ilivyosemwa:

Shaykh ana vitabu vikubwa kwa mijeledi

lakini havisomi

Unaponunua vitabu basi unatakiwa kujishughulisha kuvisoma. Wakati mke wa az-Zuhriy alipomuona ameshikilia vitabu vyake – na pengine ni mwenye kufanya upungufu katika kutangamana naye – akasema: “Naapa kwa Allaah! Vitabu vyako vinanidhuru zaidi kuliko wanavofanya wake watatu.” Namna hii ndivo anapaswa kuwa mwanafunzi! Yule anayeifanya elimu yake kuwa chini ya dunia hafikii elimu yoyote. Vivyo hivyo kuhusu ambaye anaitumia elimu au ulinganizi kwa ajili ya manufaa ya kidunia.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 497-498
  • Imechapishwa: 16/07/2025