Bora ni kufuata Sunnah na kuswali Rak´ah 11

Swali: Nikiswali kwenye msikiti ambao imamu anaswali Rak´ah ishirini – je, nikamilishe Rak´ah ishirini kwa kumfuata imamu au niswali pamoja naye Rak´ah nane na kuswali Witr peke yangu kisha niondoke zangu?

Jibu: Nakushauri kuswali Rak´ah nane na uswali Witr peke yako. Kufuata Sunnah ndio bora zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 86
  • Imechapishwa: 20/03/2024