Bora kutumia as-Salaf as-Swaalih badala ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah

Swali: Ni yepi maoni yako juu ya wale wenye kuonelea kuwa ni bora kutumia jina la as-Salaf as-Swaalih badala ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?

Jibu: Jina la Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah limedaiwa na wengi. Ashaa´irah wanajiita kuwa ndio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Vivyo hivyo ndivo wanavofanya Maaturiydiyyah. Jina la Ahl-us-Sunnah na al-Jamaa´ah ni majina mawili yanayopendwa na mazuri. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah linadaiwa na kila mmoja. Kuhusu tamko la as-Salaf as-Swaalih mtu anapambanua makusudio ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ashaa´irah, Maaturiydiyyah na wazushi wengine hawajinasibishi na jina la as-Salaf as-Swaalih. Kwa sababu wanaona kuwa njia ya Salaf ndio imesalimika zaidi lakini njia ya wale waliokuja nyuma (Khalaf) ndio wajuzi na yenye hekima zaidi. Kwa hiyo hawajinasibishi kwa as-Salaf as-Swaalih kwa sababu wamekusudia kusalimika. Kwa mujibu wao wanaona kuwa kusalimika ni kinyume na ujuzi na hekima. Ukweli wa mambo ni kwamba Salaf njia yao ndio imesalimika, elimu na hekima zaidi. kwa hiyo inatakiwa kuzinduka wakati wa kusema kwa kuachia jina la Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ni sawa baadhi ya nyakati kusema kwa kuachia pasi na kufungamanisha. Lakini kulifungamanisha baadhi ya nyakati ndio mfumo wa wanazuoni wahakiki. Mara hulisema kwa kuachia bila kulifungamanisha na wakati mwingine wanalisema kwa kulifungamanisha ili kilichoachiwa kifasiriwe juu ya kilichofungamanishwa.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://saleh.af.org.sa/sites/default/files/2017-11/16.MP3
  • Imechapishwa: 12/09/2022