Allaah aliniwekea wepesi wa kusafiri kwa ajili ya kwenda kulingania katika Tawhiyd na Sunnah. Nilisafiri katika miji ya Syria, miji ya kiarabu na baadhi ya miji ya Ulaya. Bidii yangu kubwa ilikuwa kwamba waislamu wa leo hawawezi kuokoka kutokamana na ukoloni, dhuluma na unyonge na wala hakuna faida ya ukusanyaji wa leo wa kiislamu na vyama vya kisiasa isipokuwa kwa kulazimiana na Sunnah sahihi na mfumo wa Salaf inapokuja katika ´Aqiydah, uelewa na tabia – na si juu ya yale waliyomo watu wa leo.

Allaah aliwanufaisha namna alivyotaka na wale aliowataka miongoni mwa waja Wake wema. Hayo yakadhihiri wazi katika ´Aqiydah zao, ´ibaadah zao, ujenzi wa misikiti yao, hali zao na mavazi yao. Kitu hicho kinaweza kushuhudiwa na kila mtu ambaye ana inswafu, jambo ambalo halipingwi isipokuwa tu na yule ambaye ima ana chuki au ni mwendawazimu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (7/1/616-617)
  • Imechapishwa: 07/08/2020