Swali: Kipi ambacho ni khatari zaidi: Bid´ah ya maulidi au dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa?
Jibu: Bid´ah kwa njia ya ujumla wake wanachuoni wanasema kuwa mbaya zaidi kuliko maasi. Kwa sababu mtu wa Bid´ah anaona kuwa yuko katika haki na anaendelea juu ya Bid´ah yake mpaka afe juu yake. Ama mtenda maasi anajua kuwa ni mwenye dhambi, kwamba yuko khatarini, anajutia na anatubia. Lakini mtu mwenye kufanya Bid´ah, akalazimiana nayo na akaichunga, hapana shaka kwamba anaona kuwa yuko katika haki. Kwa ajili hii kuna khatari akafa juu ya Bid´ah yake. Kwa ajili hii imekuja katika Hadiyth kwamba tawbah ya mzushi imezuiliwa mpaka atubie kutokana na Bid´ah yake.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Bid´at-ul-Mawaalid wa mahabbat-in-Nabiyy http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=36078
- Imechapishwa: 09/11/2019
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)