Kusujudu juu ya sifongo, godoro dogo au kitu mfano wake

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kuingia msikiti ambao umetandikizwa sifongo juu yake? Ni ipi hukumu ya kusujudu juu ya vitu hivyo?

Jibu: Hakuna neno kuswali katika msikiti huu. Lakini anaposujudu abonyeze juu ya sifongo hiyo mpaka itulizane. Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:

“Tulikuwa tukiswali pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Asipoweza mmoja wetu kumakinisha paji lake la uso juu ya ardhi, basi anatandaza nguo yake na anasujudu juu yake.”

Hii ni dalili inayoonyesha kwamba ni lazima kumakinisha paji la uso. Simaansihi kuwa umeweke kitu juu ya sifongo hiyo. Kwa sababu ukifanya hivo haitozingatiwa kuwa umesujudu. Kwa hivyo tunasema kwamba mtu akiswali msikitini au nyumbani kwake juu ya sifongo, basi ni lazima abonye juu yake mpaka itulizane.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58) http://binothaimeen.net/content/1328
  • Imechapishwa: 09/11/2019