Bado hadhi ya as-Swahiyh al-Bukhaariy na Muslim itabaki kuwa juu

Swali: Nimetatizwa na yaliyosemwa katika darsa ya kwamba katika “as-Swahiyh” ya Muslim kuna Hadiyth ambaz sio Swahiyh pamoja na kwamba nimewasikia wanachuoni wakisema kuwa Ummah mzima umekubaliana juu ya usahihi wa yaliyomo katika al-Bukhaariy na Muslim…

Jibu: Shaykh [al-Islaam Ibn Taymiyyah] amebainisha hilo ya kwamba vingi vilivyomo katika al-Bukhaariy na Muslim Ummah umekubaliana juu ya usahihi wake. Ina maana ya vingi vilivyomo humo. Kupatikana Hadiyth moja au mbili ambazo zimetiwa kasoro… Pengine haki iko pamoja na upande wa mwandishi au upande mwingine. Hili halidhuru usahihi wa vitabu viwili hivyo. Lau mgelikuwa mmezinduka basi Shaykh [al-Islaam Ibn Taymiyyah] amejibu hili. Amesema ya kwamba vingi vilivyomo katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na Muslim wanachuoni wamekubaliana juu ya usahihi wake. Kitendo cha kutiwa kasoro baadhi ya Hadiyth ni kitu kinachohitajia kujadiliwa; inawezekana haki iko pamoja na upande wa mwandishi kama ilivyo kwa al-Bukhaariy na inawekana vilevile haki iko pamoja na huyo mwenye kuzitia kasoro kama yaliyomfika Muslim. Lakini hata hivyo hili halitii kasoro “as-Swahiyh” ya Muslim na wala halipunguzi hadhi ya “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy. Isitoshe vilevile uaminifu wavyo haupungui.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (31) http://alfawzan.af.org.sa/node/2143
  • Imechapishwa: 13/07/2020