Baba ndiye ana haki ya kutumia mali ya mwanae, si mama

Swali: Msichana kabla ya kuolewa kwake alipewa mali na akaimpa mama yake ambapo mama yake alizitumia. Je, inajuzu kwa mama kufanya hivo?

Jibu: Hapana, haijuzu. Hizi ni pesa za msichana na haijuzu kwa mama kuzitumia isipokuwa kwa idhini yake. Baba ndiye ana haki ya kuchukua katika mali ya mtoto wake midhali haimdhuru mtoto na hahitajii. Hii ni haki ya baba tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (56) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-12-30.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020