Baba anawaamsha wanawe kuswali Fajr kwa maneno mazito

Swali: Baba yangu wakati anapotuamsha katika swalah ya  Fajr anatuita kwa kusema “Ee makafiri!”, “Ee mayahudi, amkeni mkaswali!”. Tunaomba umpe nasaha kwa kuwa anatutukana kwa maneno yasiyosemwa na Muislamu. Ni ipi nasaha yako kwake na kwangu?

Jibu: Ni juu yenu kuwa na subira. Lakini amkeni na sio mnabaki kitandani na mnamkasirisha. Hasemi hivi isipokuwa ni kwa sababu ya khasira. Nyinyi harakisheni kuamka ili asitamke matamshi kama haya. Msimkasirishe. Pamoja na hivyo haijuzu kwake kutamka kwa matamshi kama haya. Lakini inawezekana ni kwa sababu ya khasira na hivyo akawa amesema hivo kwa nyinyi kusababisha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (42) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-3-22.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020