Swali: Baba akimlazimisha mtoto wake kumtaliki mke wake. Je, ni lazima kwa mtoto kumtii katika jambo hilo?
Jibu: Hapana, si lazima kwake kufanya hivo. Halazimiki kumtii katika kumwacha mke wake ikiwa hataki jambo hilo. Asimlazimishe juu ya jambo hilo.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (39)
- Imechapishwa: 10/06/2023