Maoni yangu juu ya suala hili lina ubainifu wa nukta mbili:

1 – Inahusiana na yule mgombea

2 – Inahusiana na yule anayempigia kura.

Sipendekezi mgombea kugombea. Nina uzowefu wa hilo Syria na hivi sasa karibuni Amman pia. al-Ikhwaan al-Muslimuun wamekusanya ujasiri na wameanza kugombea. Nilikuwa nikiulizwa swali hili. Jibu langu lilikuwa sipendekezi kwa muislamu yeyote kugombea, kwa sababu kitendo hicho kinaenda kinyume na Shari´ah ya Kiislamu kwa njia nyingi:

1 – Mbaya zaidi ni kwamba mgombea anaitakasa nafsi yake wakati anapogombea kwa ajili ya kuketi katika bunge.

2 – Anajiweka mwenyewe kula kiapo cha kuheshimu kanuni. Hivyo anakuwa mwenye kwenda kinyume na Shari´ah.

3 – Yule mwenye kukaa bungeni ambayo kanuni zake zinaenda kinyume na Shari´ah na ambaye ana malengo ya kuleta mabadiliko muda unavokwenda basi yeye mwenyewe atakuja kubadilika. Mbora mzuri ni kwamba tumeona namna ambavyo mtu ana mazowea ya kuvaa mavazi ya kiarabu ambayo ni kanzu. Syria wanaiita kuwa ni ´jalabiyyah`, Yordani wanaiita kuwa ni ´dishdaash`. Pengine kichwani mwake pia anavaa kilemba cheupe. Muda unavoenda mtu akabadilika kikamilifu. Akavua kanzu na akavaa koti na suruwali. Anapotoka nje ya bunge anakuwa mtu mwingine kinyume na yule ambaye aliingia bungeni. Ni kwa nini ameingia bungeni? Ili aweze kuleta mabadiliko. Kinyume chake yeye ndiye amebadilika. Isitoshe hakuweza kuleta mabadiliko yoyote.

Sipendekezi yeyote agombee, ni mamoja ni Salafiy, Ikhwaaniy au mwingine yeyote. Kwa sababu bila shaka yoyote atadhurika kwa ugombeaji wake huu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (31) Dakika: 18.35
  • Imechapishwa: 10/08/2022