Swali: Ni ipi hukumu ya kumwita fulani haji fulani na bwana fulani (السيد فلان)?

Jibu: Kusema haji fulani anachokusudia ni kuwa amekwishatekeleza hajj. Hakuna neno.

Kuhusu bwana, basi kutatazamwa kama kweli mtu huyo ana ubwana basi kutasemwa bwana (سيد) pasi na (الـ). Hakuna vibaya kufanya hivo kwa sharti asiwe mtenda madhambi wala kafiri. Akiwa ni mtenda madhambi au kafiri basi haijuzu kusema kwa kuachia isipokuwa mtu aegemeze kwa watu wake. Kwa mfano bwana wa wana fulani, bwana wa watu fulani na mfano wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Manaahiy al-Lafdhwiyyah, uk. 50-51
  • Imechapishwa: 09/08/2022