Swali: Kuna mtu amenunua ardhi na akanuia nafsini mwake kwamba ataiuza pale itapopanda thamani yake. Pengine akabaki nayo miaka kadhaa. Je, analazimika kuitolea zakaah ilihali hajaanza kuitafutia soko?

Jibu: Amekwishanuia kwamba ikipanda bei ataiuza. Hii ndio nia ya biashara. Kwa hivyo anatakiwa kuitolea zakaah kila mwaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (16)
  • Imechapishwa: 26/04/2021