Swali: Je, ni sahihi kuwa ni Murji-ah ndio hawamfanyii Takfiyr yule asiyeswali kwa sababu ya uzembe na uvivu na kwamba Salaf walikuwa wanaonelea asiyekuwa na rai hii ametumbukia katika utata wa Murji-ah?

Jibu: Hapana. Haijuzu. Kuna wanachuoni wanaoonelea kuwa swalah ya mkusanyiko sio wajibu au mwenye kuacha swalah hakufuru maadamu hakanushi uwajibu wake. Baadhi ya wanachuoni wanaoonelea kuwa asiyeswali pasi na kukanusha uwajibu wake hakufuru. Hata hivyo kauli hii ni dhaifu. Maoni sahihi na yenye nguvu ni kwamba mtu anakufuru na ni kufuru inayomtoa katika Uislamu. Ni kauli hii ndio inayosapotiwa na dalili. Mwenye kwenda kinyume katika suala hili ni mwenye kukosea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo%20%20-%2021%20-%2008%20-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015