Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema ikiwa mtu hawakufurishi manaswara kwa kutofikiwa na Aayah iliyoko katika Suurat-ul-Maaidah:

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ

“Hakika wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni watatu wa utatu.” (05:73)

hakufurishwi mpaka afunzwe Aayah hii?

Jibu: Hajafikiwa na Aayah hii?! Hili linahitajia ufafanuzi. Ikiwa mtu huyu hajui hukumu kama hii na wala hajui kuwa manaswara wako katika batili, basi mtu huyu ni lazima kumsimamishia hoja. Ama ikiwa anajua hili na anajua vilevile kuwa manaswara wako katika batili na kwamba Allaah na maandiko [ya Qur-aan na Sunnah] yamewakufurisha, ni kafiri kwa sababu hakukanusha kufuru.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4735
  • Imechapishwa: 17/11/2014