Swali: Maneno haya ni sahihi ya kwamba ´mwenye kusema imani ni kauli, ´amali na I´tiqaad, inazidi na inapungua` atakuwa amejitenga mbali na Irjaa´ yote hata kusema kuwa mtu hakufuru isipokuwa mpaka aamini na kukanusha?

Jibu: Sentesi ya maneno ya pili yanavunja sentesi ya maneno ya kwanza. Maneno yake kuwa imani ni kauli, ´amali na I´tiqaad na kwamba inazidi na inapungua, akiwa na maana ya kwamba ni kauli ya ulimi na ya moyo, ´amali ya moyo na ya viungo na inazidi kwa utiifu na inapungua kwa maasi, hii ni haki na ndio kauli ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Lakini hata hivyo sentesi ya maneno yake ya pili kwamba mtu hakufuru mpaka aamini na kukanusha, sentesi hii inavunja sentesi ya maneno ya kwanza. Kama jinsi imani inakuwa kwa kauli, ´amali na I´tiqaad, vilevile kufuru inakuwa kwa kauli, ´amali na I´tiqaad. Hivyo, sentesi ya maneno ya kwanza yanavunja sentesi ya maneno ya pili. Ni lazima kusahihisha sentesi ya maneno ya pili na badala yake aseme ´imani inakuwa kwa kauli, ´amali na I´tiqaad` na kufuru inakuwa kwa ´kauli, ´amali na I´tiqaad`. Namna hii ndio itakuwa sahihi. Ama maneno haya yakibaki kama jinsi yalivo, sentesi ya maneno ya kwanza yatakuwa yanavunja sentesi ya maneno ya pili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4735
  • Imechapishwa: 17/11/2014