´Arshi ni yenye kumbeba Allaah?  

Swali: Wenye kubeba ´Arshi wanabeba ´Arshi tu au wanabeba ´Arshi na walio juu yake au haijuzu kuingia kwa undani katika hilo?

Jibu: Wewe umeshaingia ndani katika hili. Iko wapi faida ya kuuliza tena? Achana na hili. Tunaamini kuwepo kwa ´Arshi, tunaamini wanaoibeba na tunaamini kuwa Allaah Amelingana juu ya ´Arshi kama ilivothibiti na wala hatuingii kwenye masuala kama haya. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah anasema:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

“Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.” (20:05)

Mwenye kufikiria kuwa ´Arshi inambeba amesema uongo. Allaah ndiye mwenye kuzuia mbingu na ardhi visianguke. Yeye ndiye mwenye kuizuia ´Arshi, mbingu na ardhi (Subhaanahu wa Ta´ala). Haina maana ya kuwa yenyewe ndio inamzuia au inambeba (Subhaanahu wa Ta´ala). Lakini hata hivyo kuingia kwa undani katika hili hakuna haja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-10-30.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020