Kabla ya mtu kujenga maoni yake juu ya mada fulani, basi ni lazima kwake kutafiti na wanazuoni ambao yeye anajua kuwa ni wanazuoni. Si kupitisha maoni yake mwenyewe na akaondoka kwa hamasa, hisia na ikhlaasw, kwa sababu ikhlaasw pekee haitoshi. Kabla ya kujiingiza katika kitendo anapaswa kukisoma na wanazuoni. Najua kwamba mojawapo ya changamoto kubwa zinazowakumba waislamu ulimwenguni leo, khasa vijana wa Kiislamu, ni kupitisha maoni ambayo wameyapenda bila kuzingatia misimamo ya wanazuoni wa zamani au wa sasa. Si tu wanazuoni wa zamani, bali pia wa sasa. Masuala haya yanapaswa kuchunguzwa kwa usawa, bila mwelekeo wa kihisia au upendeleo, na kupitia ushirikiano wa kina wa kuyasoma na kuyatafakari kabla ya kuyatekeleza. Huo  ndio ushauri wangu kwa waislamu leo katika mambo yote kwa jumla na khaswa mambo yanayohusiana na jamii nzima.

  • Mhusika: Immaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´abr-al-Haatif was-Sayyaarah (2)
  • Imechapishwa: 09/12/2024