Swali: Katika swalah ya ijumaa tunapokuwa katika safari au jangwani inafaa kwetu kama watu kumi kuswali swalah ya ijumaa?
Jibu: Kwa mujibu wa dalili za Qur-aan na Sunnah, sioni kinachokataza kufanya hivyo. Kwa sababu baadhi ya masharti yaliyowekwa na baadhi ya maimamu ni ya Ijtihaad tu, na hazina dalili za moja kwa moja kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Zaidi ya hayo ni kwamba naona ndani yake kuna baadhi ya maoni yanayopingana na fataawaa zilizotolewa na maimamu wa Salaf na makhaliyfah wao wema. Katika vitabu vingi vya Fiqh, imeandikwa kwamba watu wa mashambani wanaohamahama hawawajibiki kuswali swalah ya ijumaa. Kinachokusudiwa ni kwamba imesihi kwamba khaliyfah mwadilifu ´Umar bin ´Abdul-´Aziyz aliwaandikia baadhi ya makabila yaliyokuwa yamekaa bondeni au mahali pa kuchunga kwamba watekeleze swalah ya ijumaa. Isitoshe hakuna dalili inayoondoa ueneaji wa wa maneno Yake (Ta´ala):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ
“Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya swalah siku ya ijumaa, basi kimbilieni kumtaja Allaah na acheni biashara. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua!”[1]
Adhana ya ijumaa ikitangazwa mahali popote, basi inatakiwa kufanyia kazi maneno Yake (Ta´ala):
فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ
”… basi kimbilieni kumtaja Allaah… ”
Hakukuwekwa sharti nyingine yoyote si katika Aayah wala Sunnah isipokuwa Mkusanyiko.
[1] 62:9
- Mhusika: Immaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa ´abr-al-Haatif was-Sayyaarah (2)
- Imechapishwa: 09/12/2024
Swali: Katika swalah ya ijumaa tunapokuwa katika safari au jangwani inafaa kwetu kama watu kumi kuswali swalah ya ijumaa?
Jibu: Kwa mujibu wa dalili za Qur-aan na Sunnah, sioni kinachokataza kufanya hivyo. Kwa sababu baadhi ya masharti yaliyowekwa na baadhi ya maimamu ni ya Ijtihaad tu, na hazina dalili za moja kwa moja kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Zaidi ya hayo ni kwamba naona ndani yake kuna baadhi ya maoni yanayopingana na fataawaa zilizotolewa na maimamu wa Salaf na makhaliyfah wao wema. Katika vitabu vingi vya Fiqh, imeandikwa kwamba watu wa mashambani wanaohamahama hawawajibiki kuswali swalah ya ijumaa. Kinachokusudiwa ni kwamba imesihi kwamba khaliyfah mwadilifu ´Umar bin ´Abdul-´Aziyz aliwaandikia baadhi ya makabila yaliyokuwa yamekaa bondeni au mahali pa kuchunga kwamba watekeleze swalah ya ijumaa. Isitoshe hakuna dalili inayoondoa ueneaji wa wa maneno Yake (Ta´ala):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ
“Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya swalah siku ya ijumaa, basi kimbilieni kumtaja Allaah na acheni biashara. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua!”[1]
Adhana ya ijumaa ikitangazwa mahali popote, basi inatakiwa kufanyia kazi maneno Yake (Ta´ala):
فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ
”… basi kimbilieni kumtaja Allaah… ”
Hakukuwekwa sharti nyingine yoyote si katika Aayah wala Sunnah isipokuwa Mkusanyiko.
[1] 62:9
Mhusika: Immaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa ´abr-al-Haatif was-Sayyaarah (2)
Imechapishwa: 09/12/2024
https://firqatunnajia.com/safari-ya-ijumaa-mtu-anapokuwa-safarini/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)