Answaar-us-Sunnah kazi yao ni kuwapiga vita Salafiyyuun

Baada ya kubadilika hali za Answaar-us-Sunnah Sudan na wakajishughulisha na kukusanya pesa na ikawa kazi yao ni kuwapiga vita Ahl-us-Sunnah – yaani vijana wenye kushikamana na dini ambao wanawakemea jambo la kuchanganyika wanaume na wanawake kwenye vyuo na kuwakemea vilevile kitendo cha wao kujenga misikiti na kuisalimisha kwa Suufiyyah. Vijana wenye kushikamana na dini wanatakiwa kukimbia mbali na wao kwelikweli.

Sisi tunawanasihi kujitenga mbali na kundi la Answaar-us-Sunnah. Wamekuwa hawana shughuli nyingine isipokuwa kukusanya pesa. Tunamuomba Allaah awarudishe katika haki kwa njia nzuri.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Makhraj min al-Fitnah, uk. 133-134
  • Imechapishwa: 26/08/2020