Ahl-ul-Bid´ah ni wenye madhara zaidi kuliko makafiri

Wanasema – Ahl-ul-Bid´ah – ya kwamba sisi tunasema kuwa wao wana madhara makubwa kwa waislamu kuliko mayahudi na manaswara. Maneno haya wanayanasibisha kwa Rabiy´ peke yake. Pamoja na kwamba sisi tumewaletea [dalili ya hilo] mara kwa mara, kuanzia kwa yale tuliyoandika, na khaswa kitabu cha karibuni “al-Mahajjat-ul-Baydhwaa´”. Humo tumenukuu kutoka kwa wanachuoni saba wa Uislamu waliosema kuwa Ahl-ul-Bid´ah ni wenye shari zaidi juu ya Uislamu na Waislamu kuliko makafiri. Ni kwa nini twasema hivo? Tumefafanua maneno haya mara kwa mara na nafikiri kuwa tumebainisha hilo katika kitabu hichi. Hilo ni kwa sababu Waislamu wanadanganyika na Ahl-ul-Bid´ah, kama alivosema Ahmad (Rahimahu Allaah), ambayo amekutajieni ndugu yetu Hamad.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/site/audios/HamadOthman/Divers/05Rabee01.mp3
  • Imechapishwa: 26/08/2020