Ninawausia ndugu zangu wajipambe kwa tabia hii nzuri. Hekima sikusudii kufanya Tamyi´

katika mambo, kuyatumia vibaya, kupakana mafuta na mfano wa hayo. Mambo haya yanapelekea kuiangamiza Da´wah na yanaingia katika al-Mudaahanah ambako Allaah Amesema juu yake kumwambia Mtume mtukufu:

وَدُّوا لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ

“Wanatamani lau kama ungelilainisha nao pia walainishe.” (68:09)

Wanachuoni wanasema haina neno kufanya al-Mudaaraat. Ni kuacha sehemu ya dunia yako kwa ajili ya dini. Ama al-Mudaahanah ni kuacha dini kwa ajili ya dunia na yenye kufungamana nayo. Hivyo basi, tuwe na tahadhari sana na kufanya al-Mudaahanah na Tamyi´ katika Da´wah.

Ni sawa wakati fulani mtu akafanya ukali kwa kiasi wakati anapolingania katika dini ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) sehemu kutapohitajika kufanya hivo. Sio kufanya hivyo katika sehemu zote. Mwenye kufanya upole ndio mfumo wake wa siku zote, huyu ataiharibu Da´wah. Mwenye kufanya ukali ndio mfumo wake wa siku zote, huyu pia ataiharibu Da´wah. Kila kitu kina nafasi yake. Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Amesema:

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ

“Muhammad ni Mtume wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri; wanahurumiana kati yao.” (48:29)

Na sifa nyinginezo ambazo Allaah amemsifu Mtume Wake na Maswahabah zake watukufu. Tunachotaka kulenga ni kwamba ukali wakati mwingine unahitajika kwa makafiri. Hata kwa watenda maasi Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) wakati mwingine amesema kuwafanyia ukali.

الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا مِائَةَ جَلْدَةٍ ۖ وَلَا تَأْخُذْكُم بِهِمَا رَأْفَةٌ فِي دِينِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ وَلْيَشْهَدْ عَذَابَهُمَا طَائِفَةٌ مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ

“Mzinifu mwanamke [asiyeolewa] na mzinifu mwanamme [asiyeoa], mpigeni kila mmoja katika wawili hao bakora mia na wala isiwashikeni kwa ajili yao huruma katika dini [kupitisha Shari’ah] ya Allaah mkiwa nyinyi mnamwamini Allaah na siku ya Mwisho. Na washuhudie adhabu yao [ya kupigwa mijeledi] kundi la waumini.” (24:02)

Mzinifu tunampiga bakora mia [ikiwa hajawahi kuoa au kuolewa] na tunampiga mawe [ikiwa aliwahi kuoa au kuolewa] mpake afe. Hakuna nafasi hapa ya kufanya huruma wala upole. Kila kitu kina mahala pake stahiki.

Vilevile mlevi anapigwa bakora. Mwizi anakatwa mkono. Hakuna nafasi ya huruma hapa. Watu walimuhurumia mwanamke anayetokana na kabila la Banuu Makhzuum [ambaye alikuwa anataka kukatwa mkono kwa kuiba] na wakataka kumuombea kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakasema hakuna awezae kumuombea isipokuwa Usaamah bin Zayd. Akaenda kumuombea ili mwanamke anayetokana na kabila la Banuu Makhzuum asikatwe mkono wake. Akasema “Je, unataka kuzuia adhabu miongoni mwa adhabu za Allaah? Ninaapa kwa Allaah lau ingelikuwa ni Faatwimah bint Muhammad ndiye ameiba ningelimkata mkono wake. Wakati fulani ni lazima kuwepo ukali kama huu.

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ جَاهِدِ الْكُفَّارَ وَالْمُنَافِقِينَ وَاغْلُظْ عَلَيْهِمْ ۚ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ

“Ee Nabii! Pambana na makafiri na wanafiki na kuwa mshupavu kwao. Na makazi yao ni [Moto wa] Jahannam – na ubaya ulioje mahali pa kuishia!” (09:73)

Kila kitu kina mahala pake stahiki.

Mwenye hekima ni yule anayeyaweka mambo mahala pake. Hakuna upole unaoilegeza Da´wah na kufanya unaiharibu Da´wah kama ambavyo hakuna ukali unaofanya kuwakimbiza watu. Muumini siku zote anakuwa kati na kati. Mpaka hatimaye anahakikisha Da´wah inaenea kwa watu kwa njia ilio nzuri.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/site/audios/HamadOthman/Divers/05Rabee01.mp3
  • Imechapishwa: 26/08/2020