Anayepapasa kwenye madirisha au milango ya Haram

Swali: Vipi kuhusu mtu anayepapasa kwenye madirisha au milango ya msikiti Mtakatifu na kuamini kuwa hii ni ´ibaadah inayomkurubisha mbele ya Allaah?

Jibu: Hii ni Bid´ah. Akiwa na imani juu ya jambo hilo na akayaomba inakuwa shirki. Lakini kule kudhani tu kuwa ni ´ibaadah na kitendo chema ni Bid´ah. Anapaswa kufunzwa.

Swali: Je, anapaswa akaripiwe?

Jibu: Anapaswa kukemewa na kufundishwa kwamba ni Bid´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31470/ما-حكم-التمسك-بنوافذ-او-ابواب-الحرم
  • Imechapishwa: 30/10/2025