Ni lini zinaanza Takbiyr zilizofungamanishwa kwa anayefanya hajj?

Swali: Takbiyr iliyofungamana kwa upande wa anayefanya hajj?

Jibu: Inaanza baada ya Dhuhr ya siku ya kuchinja, kwa sababu anakuwa ameshughulishwa na Talbiyah. Anapokuwa ameingia katika Ihraam anakuwa akijishughulisha na Talbiyah, jambo ambalo ndio bora zaidi. Lakini hapana vibaya akileta Takbiyr. al-Bukhaariy na Muslim wamepkea kwamba Anas amesema:

“Miongoni mwetu walikuwa wapo wanaotamka Talbiyah na hawakusemwa vibaya na wapo wanaotamka Takbiyr na hawakusemwa vibaya.”

Hapo ni pale walipokuwa wakielekea ´Arafah pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini Talbiyah ndio bora zaidi katika hali hii, kwani ndiyo nembo ya Hajj.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31493/متى-يبدا-التكبير-المقيد-بالنسبة-للحاج
  • Imechapishwa: 30/10/2025