Swali: Je, ahukumiwe yule ambaye anajuzisha kuwafanyia Khuruuj [uasi] watawala kuwa ni Khaarijiy na apewe Ahkaaam za Khawaarij?

Jibu: Ndio. Yule ambaye anaita kuwafanyia uasi watawala kwa njia hii ya Khawaarij, yeye ni katika wao. Miongoni mwao pia ni wale wanaowachochea vijana na Ummah kufanya uasi na kumwaga damu na kuhalalisha heshima zao, kuiharibu Dini na kuudhoofisha Ummah wa Kiislamu – kama Algeria na kwenginepo – huyu ni mbaya zaidi kuliko Khawaarij. Na ni wajibu kutahadhari na mtu huyu na kutahadharisha watu dhidi ya mtu huyu na kumpiga vita katika kila tovuti na kila mahala. Watu hawa ni maadui wa Allaah na Uislamu. Wanawaingiza watu katika maangamivu. Pengine ni maadui wa Uislamu wanaotumiwa na Mayahudi na Manaswara ambao wanawasaidia. Wao ndio wanawatuma kwa machafu kama haya. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema kuwahusu walio bora kuliko wao:

“Ni shari ya viumbe, laiti nikikutana nao nitawaua kama walivyouawa watu wa ´Aad.”

Watu hawa Khawaarij ambao Mtume kasema hivi kuwahusu, wao ni bora zaidi kuliko watu hawa kutokana na kupinda kwao na madhara yao, ambao wameeneza fitina na kusababisha kufa kwa Waislamu. Badala ya wao kupitia njia ya Ahl-us-Sunnah, kwa kuwanasihi watu kwa hekima na kuwafunza elimu yenye manufaa na kuwapa tarbia nzuri sahihi, tumekuja kupata watu wapumbavu, wajinga, Hizbiyyuun, na wamwagaji wa damu. Allaah Awaangamize. Na tunamuomba Allaah Auhifadhi Ummah kwa shari yao. Ummah umekuwa hauna watu wa shari kama watu sampuli hii wanaojipamba kwa Uislamu na pengine hata ni katika kampeni za maadui. Tunamuomba Allaah Auhifadhi Ummah kutokana na woa.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/catplay.php?catsmktba=355