Anayefikiwa na tajrama ya Qur-aan imemsimamikiwa hoja

Swali: Qur-aan ikifanyiwa tarjama kwa lugha moja wapo ya watu. Je, watu hao wamesimamiwa na hoja?

Jibu: Ndio, wakifikiwa na maana ya Qur-aan. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ

“Nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia.”[1]

Anayefikiwa na Qur-aan amesimamikiwa na hoja.

[1] 06:19

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/
  • Imechapishwa: 31/01/2020