Anaweza kuswali swalah tano kwa wudhuu´ aliyonuia swalah moja?

Swali: Malengo ya kutia nia wakati wa kutawadha kunakusudiwa kwamba mtu anuie kuswali swalah maalum?

Jibu: Hapana, sio lazima unuie swalah maalum. Tawadha kwa ajili ya kuondosha hadathi, sawa ikiwa utaswali au hautoswali.

Swali: Nikitawadha kwa nia ya kuswali swalah moja kisha kwa wudhuu´ huo huo nikaswali swalah tano ni sawa?

Jibu: Unaweza hata ukaswali nao swalah mia. Haina neno. Ukiondosha hadathi na wudhuu´ bado umebaki na haujatenguka swali upendavyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (04) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh–14340323.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020