Anataka jina la Allaah baada ya kumtuma mbwa wa mawindo

Swali: Je, kiwandwa kinakuwa ni halali kwa ambaye amekumbuka kutaja jina la Allaah punde tu kabla ya mbwa wa mawindo kukamata kiwindwa?

Jibu: Hapana. Anatakiwa kutaja pale anapomwagiza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ukimwagiza mbwa wako aliyefunzwa na ukataja jina la Allaah, basi kula.”[1]

Bi maana pale unapomtuma. Hafai na haitoshi kutaja jina la Allaah baada ya kwamba umeshamtuma mbwa.

[1] Muslim (1929).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (41)
  • Imechapishwa: 16/11/2023