Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Yule mwenye kuapa na akasema:

“Mimi najitenga mbali na Uislamu.”

Akiwa ni mwongo basi mambo ni kama alivosema na akiwa ni mkweli basi hatorudi katika Uislamu akiwa salama.”[1]

Je, anatoka nje ya Uislamu?

Jibu: Ni kwa njia ya matishio.

Swali: Kwa hivyo hakufuru?

Jibu: Hapana. Ni kwa njia ya makemeo. Ni kama kama alivosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kuapa kwa amana si katika mimi.”

Ni kwa njia ya makemeo:

“Si katika mimi yule atayejipiga mashavu, akapasua nguo na akaita wito wa kipindi cha kikafiri.”[2]

[1] Abu Daawuud (3258) na tamko ni lake, an-Nasaa´iy (3772), Ibn Maajah (2100) na Ahmad (23006).

[2] al-Bukhaariy /(1212) na tamko ni lake, na Muslim (148).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22060/معنى-حديث-ان-كان-كاذبا-فهو-كما-قال
  • Imechapishwa: 25/10/2022