01. Hadiyth “Siku moja wakati Mtume wa Allaah alikuwa akikhutubia… “

280 – Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

يبنما رسول الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – يخطب يوماً، إذ رأى نُخامةً في قِبلةِ المسجدِ، فتغيظَ على الناسِ، ثم حكَّها، -قال: وأحسبُهُ قال:- فدعا بِزَعفَرانٍ فَلَطَخَهُ به وقال:

“إنّ الله عز وجل قِبَلَ وجه أحدكم إذا صلّى، فلا يَبصق بين يديه”

“Siku moja wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikhutubia aliona makohozi upande wa Qiblah cha msikiti. Akawakasirikia watu kisha akayasugua. Nadhani kuwa aliitisha zafarani na akaipaka halafu akasema: “Hakika Allaah (´Azza wa Jall) yuko upande wa Qiblah cha mmoja wenu anaposwali. Hivyo msiteme mate mbele yenu.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuud na upokezi ni wake.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/232)
  • Imechapishwa: 25/10/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy