Swali: Je, inajuzu kwangu kutembelea kaburi la baba yangu au inatosheleza kumuombea du´aa na kumtolea swadaqah kwa kuwa ninahisi kama ninafanya upungufu juu ya haki ya babangu pale ambapo simtembelei makaburini?

Jibu: Yote mawili yakiwezekana kwa wewe kumtembelea na kumuombea, vilevile kumtolea swadaqah, hili ni bora. Ikiwa hukuweza kumtembelea, inatosheleza kumuombea du´aa na kumtolea swadaqah na kumuombea msamaha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-2-10.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020