an-Najmiy kuhusu kitabu ”al-Irhaab”, ”al-Qutbiyyah” na ”Madaarik-un-Nadhwar”

Swali 09: Unasemaje kwa baadhi ya ndugu ambao wanasema kuwa kitabu “al-Qutwbiyyah”, cha muheshimiwa Shaykh Abu ´Abdillaah bin Ibraahiym bin Sultwaan al-´Adnaaniy, “Madaarik-un-Nadhwar”, cha Shaykh ´Abdul-Maalik bin Ahmad Ramadhwaaniy na “al-Irhaab”, cha Shaykh Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy, vinaeneza fitina na kuwatukana wanachuoni na walinganizi?

Jibu: Maneno yao ni batili. Vitabu hivi vinazindua makosa. Ni wajibu kwa wote kuzindua makosa haya na kutahadharisha nayo. Hatuwezi kutahadharisha makosa haya isipokuwa mpaka tusome vitabu hivi vya radd, sawa ikiwa ni vitabu hivi [vilivyotajwa] au vyenginevyo.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah ´an al-Manaahij ad-Da´wiyyah, uk. 12
  • Imechapishwa: 05/07/2020