Swali: Ni sharti kwanza kumsimamishia mtu hoja kabla ya kumzingatia mtu kuwa mzushi kwa sababu kuna watu wanajengea dalili maneno ya Shayk-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) katika ”Minhaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah” isemayo kwamba mtu kwa dhati yake hapewi hukumu ya Tabdiy´ isipokuwa baada ya kutimia masharti na kutokuwepo vikwazo. Lakini ana maneno mengine ambayo wanayajengea dalili ambao wanaona kinyume na maoni haya. Je, maneno haya ni kweli kutoka kwa Shaykh-ul-Islaam na ipi kauli yenye nguvu juu ya masuala ya Tabdiy´? Ni lazima kwanza kumsimamishia mtu hoja ili wanazuoni wamtie katika Tabdiy´ mtu kwa dhati yake?
Jibu: Kumekithiri maongezi kuhusiana na hili. Tabdiy´ haitokani na Iqaamat-ul-Hujjah. Bali mtu anatakiwa kunasihiwa. Ikiwa Bid´ah zake ziko wazi, basi anasihiwe mtu wa Bidah. Na wala hakusemwi nimemsimamishia hoja. Kumsimamishia mtu hoja inahitajika wakati tu wa kukufurisha. Kuhusu wakati wa Tabdiy´ hapana.
Wakati Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) alipomuuliza mtu akasema Ibn Abiy Qutaylah Makkah amesema kuwa Ahl-ul-Hadiyth ni watu waovu, akasema:
“Zindiyq! Zindiyq! Zindiyq!”
Alikuwa akitoa vumbi kwenye nguo yake kwa mikono na huku akisema:
“Zindiyq! Zindiyq! Zindiyq!”
Hakusema kwanza itabidi nimsimamishie hoja. Kumfanyia mtu Tabdiy´ si sharti kwanza kumsimamishia mtu hoja.
- Muhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=127300
- Imechapishwa: 05/11/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)