Ameweka nadhiri watoto wake wasifanye kitu fulani ambapo wakamkhalifu

Swali: Kuna mwanamke aliwaambia watoto wake:

“Ni juu yangu nadhiri mkifanya kitu fulani.”

Baadaye wakafanya kile kitu japokuwa hakukitaja jina. Ni kipi kinachomlazimu?

Jibu: Kitu cha kwanza tunamkataza jambo la nadhiri. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameikataza na akasema:

“Haiji kwa kheri. Hairudishi nyuma kilichopangwa.”

Hali imefikia kiasi cha kwamba wapo wanachuoni walioharamisha nadhiri. Kwa sababu mtu anailazimisha nafsi yake kisichomlazimu.

Pili kuhusiana na qadhiya ya mwanamke huyu analazimika kutoa kafara ya yamini. Kwa sababu nadhiri hii hukumu yake ni ya kiapo. Hivyo anatakiwa kuwalisha masikini kumi au awavishe au aache mtumwa huru. Asipopata basi afunge siku tatu mfululizo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (74) http://binothaimeen.net/content/1721
  • Imechapishwa: 23/08/2020