Swali: Ni lazima kwa ambaye anafundisha ndani ya misikiti ya Ahl-ul-Bid´ah kuwatajia waziwazi makosa yao?

Jibu: Ikiwa hilo litapelekea kuzuiwa kufanya darsa, bora ni yeye kuendelea kusomesha na asitaje kitu kitachopelekea akazuiwa. Lakini hata hivyo anapaswa kubainisha haki pasi na kutaja makosa yao ili asije kufukuzwa mahali hapo. Ikiwa uwepo wake hapo itamfanya yeye kusema na kubainisha haki na jengine watu wanafaidika kutoka kwake na endapo atazungumzia makosa yao watamfukuza na kumzuia, basi faida haitopatikana. Lakini hata hivyo atatakiwa kuwabainishia makosa yao wao wenyewe. Atatakiwa kuzungumza nao na asiwabainishie ndani ya darsa hadharani mbele za watu na matokeo yake akaja kuzuiwa kufanya darsa ambayo ndani yake mna faida na manufaa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Muwattwa’ (26)
  • Imechapishwa: 23/08/2020