Anachozingatia Allaah ni nyoyo na matendo ya watu

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah hatazami miili yenu wala mali zenu; anatazama nyoyo zenu na matendo yenu.”[1]

Nini makusudio ya kutokutazama?

Jibu: Makusudio ya kutokutazama ni kwamba hatilii umuhimu wowote. Hadiyth hii ni kama mfano wa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah hatowatazama siku ya Qiyaamah na wala hatowatakasa.”[2]

Kwa sababu ya kuwakasirikia. Yeye (Subhaanah) ni mjuzi wa kila kitu. Anakiona kila kitu. Lakini kinachokusudiwa ni mtazamo wa hali ya kuridhia na kupenda.

[1] Muslim (2564).

[2] Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Watu aina tatu Allaah hatowatazama siku ya Qiyaamah, hatowatakasa na watakuwa na adhabu kali: mwanaume mwenye kuburuta kikoi chake, mwenye kufanya masimango kwa kile alichokitoa na yule mwenye kuuza bidhaa yake kwa kiapo cha uongo.” Muslim (406).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 40
  • Imechapishwa: 23/08/2020