Amewasili katika mji wake akakusanya Dhuhr na ´Aswr

Swali: Nilisafiri kwenda Riyaadh kwa ajili ya masomo. Nilipokuwa njiani ilinipata swalah ya Dhuhr ambayo sikuiswali isipokuwa saa nane nilipofika Riyaadh ambapo nikakusanya ´Aswr pamoja nayo kutokana na ukali wa uchovu. Je, ukusanyaji huu ni sahihi?

Jibu: Ikiwa umefika Riyaadh na ukanuia kukaa huko kwa muda wa zaidi ya siku nne basi haifai kwako kukusanya. Katika hali hiyo utaswali Dhuhr peke yake na ´Aswr utaiswali pamoja na wengine. Ukitanguliza ´Aswr basi swalah hiyo ni batili. Utatakiwa kuirudi swalah yako. Lakini ukiwa msafiri ambapo umepanga kukaa siku moja, mbili, tatu au nne ni sawa ukakusanya kwa sababu unazingatiwa ni msafiri. Lakini haitakikani kwa mtu kuswali peke yake anapopata mkusanyiko.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 26/06/2021