Swali: Vipi kuhusu mtu aliyesimama ´Arafah usiku kisha akakosa kulala Muzdalifah?
Jibu: Hapana vibaya ikiwa alikuwa na udhuru. Mfano wa hili ni kama hali ya ´Urwah aliyefika Muzdalifah asubuhi ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumwamuru kutoa fidia. Lakini ikiwa mtu alikosa kwa kuzembea, basi anapaswa kutoa fidia.
Swali: Vipi ikiwa mtu atasimama ´Arafah kwa muda wa saa moja tu?
Jibu: Inamtisho ikiwa atawasili mwishoni mwa usiku.
Swali: Nini kipimo cha udhuru kwa mtu aliyekosa kulala Muzdalifah?
Jibu: Kipimo ni ukosefu wa uwezo wa kufika Muzdalifah. Mfano gari lake lilipata hitilafu na hakuweza kufika, amezuiliwa na maradhi, amepotea njia au nyudhuru kama hizo zinazokubalika kwa mujibu wa Shari´ah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25001/حكم-من-وقف-بعرفة-ليلا-ثم-فاته-المبيت-بمزدلفة
- Imechapishwa: 23/01/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Amefika Muzdalifah baada ya jua kuzama
Swali: Nilifika Muzdalifah baada ya jua kuzama kwa sababu ya msongamano mkubwa wa watu. Je, ni lazima nitoe fidia? Jibu: Ikiwa unasafiri kwenda Muzdalifah na ukazuiwa na msongamano mkubwa wa watu, hakuna kinachokulazimu. Kwa sababu ni mwenye kupewa udhuru.
In "Kubaki Muzdalifah"
29. Bid´ah za Muzdalifah
95- Kutembea kwa haraka kutoka ´Arafah kwenda Muzdalifah. 96- Kuoga kwa ajili ya kulala Muzdalifah. 97- Kupendelea kushuka kipando ili kuingia Muzdalifah kwa kutembea kwa miguu kwa ajili ya kuiheshimisha Haram. 98- Mtu kulazimiana na du´aa ifuatayo wakati anapofika Muzdalifah: اللهم إن هذه مزدلفة جمعت فيها ألسنة مختلفة نسألك حوائج…
In "Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah"
Watu wasiostahiki kujibiwa
Swali: Tulisafiri kwenda hajj na pindi tulipopanda ´Arafah gari ikaharibika mwishoni mwa ´Arafah. Baada ya kumaliza kuswali Maghrib tukatengeneza gari na kuendelea na safari. Lakini hata hivyo hatukujua njia. Tukapotea na baadaye gari ikaharibika kwa mara nyingine. Hatukufika Muzdalifah isipokuwa baada ya jua kuzama. Ni ipi hukumu? Ibn ´Uthaymiyn: Sijibu…
In "Hajj na ´Umrah"