Amerudi Minaa masaa mawili ya mwisho

Swali: Usiku wa kuamkia tarehe 11 niliswali ´Ishaa Minaa. Kisha baadaye nikaenda katika msikiti Mtakatifu ili nifanye Twawaaf-ul-Ifaadhwah. Kwa sababu ya msongamano mkubwa wa watu sikurudi Minaa isipokuwa masaa maawili kabla ya alfajiri. Kuna kinachonilazimu?

Jibu: Midhali umerudi masaa mawili ya mwisho kabla ya alfajiri, ukatumia usiku uliobaki Minaa na ukaswali Fajr hapo, inatosha – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (23) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-13-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2020