Eda ya mwanamke aliyetalikiwa ikiwa ada yake ni yenye kukawia

Swali: Kuna mwanamke amepewa talaka tatu na ada yake ya kila mwezi si yenye kuja kwa mpangilio. Anaweza kufanya mwezi mmoja mpaka miwili bila kupata ada. Ni ipi itakuwa eda ya mwanamke huyu?

Jibu: Mwanamke anayepata hedhi eda yake ni hedhi tatu. Ni mamoja muda ukawa mrefu au mfupi. Kujengea juu ya hili iwapo mtu atamtaliki mke wake baada ya kuzaa, kikawaida mwanamke anapokuwa ni mwenye kunyonyesha hapati hedhi. Katika hali hii tunasema kuwa mwanamke huyu anatakuwa kusubiri mpaka pale atapopata hedhi baada ya kumaliza kunyonyesha na apate hedhi mara tatu. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ

“Wanawake waliotalikiwa wabakie kungojea zipite hedhi  [au twahara] tatu.”[1]

Hili ndilo la wajibu.

[1] 02:228

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1496
  • Imechapishwa: 20/06/2020