Swali: Mimi nina shamba lililozungukwa na ukuta. Ndani ya ukuta mna kaburi. Mwanadani wake unaonekana juu ya ardhi. Nimewauliza watuwazima juu ya hilo wakasema kuwa kaburi liko hivo na kwamba kamwe hawalitambui. Nilipoanza kupalilia sehemu hiyo ili kupanua sehemu nikaona kuwa kuna makaburi matatu mengine. Shamba limeshapanuliwa kwenye kuta zake. Je, nimefanya kosa?

Jibu: Makaburi yanatakiwa kuheshimiwa mpaka pale maiti watapooza. Naonelea kuwa unatakiwa kwenda kwa Qaadhiy mahakamani na umwache ayaangalie hayo makaburi. Hukumu yake itakuwa nzuri – Allaah (Ta´ala) akitaka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/205)
  • Imechapishwa: 26/08/2021