Ameoa bila karamu ya ndoa

Swali: Nilioa na sikufanya karamu ya ndoa. Je, napata dhambi?

Jibu: Hapana. Umeacha jambo lililopendekezwa. Karamu ya ndoa imependekezwa. Ambaye hakufanya karamu ya ndoa ameacha jambo lililopendekezwa. Kwa hiyo hapati dhambi. Lakini akifanya karamu ya ndoa analipwa thawabu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Allaah akubariki. Fanya karamu ya ndoa ijapo kikondoo.”[1]

Huku ni kuitangaza ndoa.

[1] al-Bukhaariy (4/232), an-Nasaa’iy (2/93), Ibn Sa´d (3/2/77), al-Bayhaqiy (7/258), Ahmad (3/165) na Abul-Hasan at-Twuusiy katika ”al-Mukhtaswar” (1/110/1).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (31)
  • Imechapishwa: 12/03/2022