Amekuja kumchumbia binti yangu mtu asiye sawa

Swali: Ikiwa kuna mwanaume yuko na msichana anayefaa kuolewa na hakuna aliyekuja kumchumbia isipokuwa mwanaume asiyefaa katika dini yake. Je, amuozeshe naye?

Jibu: Hangaliwa hali yake. Ikiwa upungufu uliopo katika dini yake haujafikia ukafiri, bali ana baadhi ya maasi tu, basi hapana vibaya kumuozesha ikiwa hakupatikana aliye bora zaidi yake. Lakini ikiwa amepatikana aliye bora zaidi yake katika dini, basi aliye bora ndiye anayepaswa kutangulizwa. Ama ikiwa mambo yamekwama na hakupatikana mwenye kufaa zaidi katika dini, na aliyepatikana ni mtu mwenye baadhi ya maasi lakini si kafiri, basi hakuna tatizo kumuozesha.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1632/حكم-تزويج-البنت-من-ليس-كفىا-في-دينه
  • Imechapishwa: 28/06/2026