Amekufa kabla ya kutoa zakaah

Swali: Kuna mtu alikufa kabla ya kutoa zakaah yake. Je, dhimma yake ya inatakasika endapo watoto wake watamtolea nayo?

Jibu: Kama ameacha mirathi basi zakaah itatolewa kutoka kwenye mirathi yake. Kwa sababu ni deni liko juu yake. Deni ndilo linatakiwa kuanzwa kabla ya kugawa mirathi na wasia. Ndio haki ya kwanza iliyofungamana na mirathi baada ya kumaliza kumwandaa maiti. Deni ni jambo muhimu sana. Ama kama alikuwa hana mirathi yoyote na wakataka kumtakasia dhimma yake, jambo hilo ni katika kumtendea wema ijapokuwa sio ndugu zao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (17) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdtf-08011435.mp3
  • Imechapishwa: 05/10/2019