Swali: Kutokana na msongamano wa watu wengi katika misikiti miwili Mitukufu au misikiti mingine mikubwa, inatokea mtu anakosa viatu vyake. Baada ya kusubiri kitambo kirefu anapata viatu vengine visivyokuwa na mmiliki. Je, inafaa kwake kuvichukua?

Jibu: Ikiwa ni viatu vilivyotupwa na vilivyokusanywa kwenye takataka, haina neno. Lakini kama vimetunzwa na pengine wenye navyo wakaja kuvichukua, usivichukue.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (31)
  • Imechapishwa: 04/03/2022