Swali: Kipi kinachomlazimu kijana ambaye ameapa kabla ya Fajr kuwa hatolala kisha akajitandaza ardhini na kuanza kusoma Qur-aan na tahamaki akachukuliwa na usingizi na akaikosa swalah ya Fajr?

Jibu: Halazimiki kutoa kafara ikiwa hakukusudia kulala. Lakini kule kujitandaza kwake na kuchukulia wepesi ni katika alama za kupuuza na kukaribisha usingizi. Ambaye anaapa anatakiwa kuwa mwangalifu na kujihadhari zaidi. Vinginevyo anapaswa kutoa kafara ya kiapo kwa kuchukulia wepesi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22702/حكم-من-حلف-الا-ينام-ثم-نام-وفاتته-الصلاة
  • Imechapishwa: 03/08/2023