Amefanya ´Umrah na watoto ambao wameshindwa kufanya Sa´y

Swali: Nilifanya ´Umrah nikiwa na watoto wawili wadogo. Wakaingia ndani ya Ihraam wakiwa kwenye kituo, lakini walipoanza Sa´y walichoka. Je, kuna kitu kinanibidi kufanya?

Jibu: Unapaswa kuwabeba juu ya gari au kuwabeba mikononi wakati wa Sa´y. Watoto, ikiwa watachoka au kushindwa, mzazi wao au mlezi mwingine anaweza kufanyisha Twawaaf na Sa´y. Awasaidie kukamilisha.

Swali: Sikuwafanya Sa´y kwa niaba yao. Je, hivi sasa kuna jambo linalonilazimu?

Jibu: Udhahiri ni kwamba unapaswa kurudi na kuwafanyisha Sa´y, kwa sababu wewe ndiye umejilazimisha kwao na ukaingia nao ndani ya Ihraam. Kwa hivyo unapaswa kumalizia´ibaadah yao, kufanya nao Sa´y na kupunguza nywele kwa niaba yao. Amesema (Ta´ala):

وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّـهِ

“Timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah. “[1]

Wewe ndiye uliyewaingiza katika ´ibaadah hiyo.

[1] 02:196

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24965/ماذا-يلزم-من-اعتمر-ومعه-طفلان-لم-يسعيا
  • Imechapishwa: 14/01/2025