Ni wajibu kwa watoto wadogo kukamilisha Hajj na ´Umrah?

Swali: Je, maneno Yake Allaah:

وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّـهِ

“Timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah. “[1]

yanawahusu mpaka watoto wadogo?

Jibu: Inawahusu wale walioingizwa katika ´ibaadah na walezi wao, lakini wao wenyewe hapana. Hakuna kinachowalazimu ikiwa walijiingiza wenyewe. Hata hivyo ikiwa mlezi wao ndiye aliyewaingiza, hili ndio suala ambalo wanalizungumzia wanazuoni. Ikiwa mlezi aliwaingiza watoto walio chini ya umri wa miaka saba, basi ni wajibu kwake kuwasaidia kumaliza ´ibaadah hiyo. Ikiwa watoto walijiingiza wenyewe katika Ihraam, wanaweza kujitoa katika Ihraam, lakini inapendekezwa mlezi wao awafundishe na awasaidie kukamilisha ´ibaadah hiyo, hata kama hawawajibiki kufanya hivyo kwa sababu hawajafikia umri wa kuwajibika. Mtu anaweza kusema pia kuwa ni wajibu kukamilisha kwa sababu walijiingiza wenyewe katika ´ibaadah hiyo, kama ilivyo kwa mtu anayefanya Hijjah au ´Umrah ya khiyari. Lau mtu ataingia ndani ya Hajj au ´Umrah ya kujitolea, basi ni lazima akamilishe. Hukumu hiyohiyo inaweza kusemwa juu ya mvulana kwmaba ni lazima kwa mlezi kuhakikisha wanakamilisha ´ibaadah hiyo, kwa sababu yeye ndiye aliyewaingiza. Haijalishi kitu hata kama watoto hao hawajawajibika kwa mujibu wa Shari´ah. Ni jambo lililozuka. Ni kama jinsi watoto wanavyokatazwa kufanya madhambi, ingawa hawawajibiki kwa mujibu wa Shari´ah, ili wasizowee au kutofanya mambo kiholela. Haya ndio maoni yenye nguvu. Lakini kimsingi ni kwamba watoto hawawajibiki kwa sababu hawajafikia umri wa uwajibikaji. Hata hivyo ikiwa watoto hao ni wenye akili na wana umri wa miaka saba au zaidi, inapaswa kwa mlezi wao kuwasisitiza wakamilishe ´ibaadah hiyo. Na ikiwa mlezi ndiye aliyewaingiza wakiwa chini ya umri wa miaka saba, basi ni wajibu kwake kukamilisha ´ibaadah hiyo kwa niaba yao, kwa kuwa yeye ni mwenye kuwajibika juu yao, kama vile anavyowazuia wasifanye mambo ya haramu.

[1] 02:196

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24966/هل-يجب-على-الصغار-اتمام-الحج-والعمرة
  • Imechapishwa: 14/01/2025